Karibu

Mpendwa mteja wetu

Unakaribishwa sana kwenye Tovuti ya ‘Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani’. Tovuti hii inatumika kama kiolesura cha kawaida ambapo wateja wetu wapendwa wanaweza kupata uelewa wa Bonde na utendaji kazi wake, kupata huduma/bidhaa zetu, kubadilishana taarifa muhimu, kutoa maoni, kujadili changamoto, kuleta fursa na kupendekeza mbinu bora ya kusonga mbele ili tufikie lengo letu la pamoja la kusimamia Rasilimali za Maji kwa njia endelevu. Ni imani yetu kuwa uwepo wa tovuti hii utaongeza ushiriki wa wadau katika ulinzi na uhifadhi wa vyanzo vya maji kulingana na kauli mbiu yetu ambayo inasema

“Utunzaji wa vyanzo vya Maji ni Jukumu letu sote”