i. Umakini kwa Wateja
Wafanyakazi wa Bonde la Pangani daima watatoa huduma bora kuzidi matarajio ya wateja
ii. Uwajibikaji
Watumishi wa Bonde la Pangani watafanya kazi zao kiushindani kwa weledi, uwajibikaji, kujituma na kwa uwazi wa hali ya juu.
iii. Uzalendo
Wafanyakazi wa Bonde la Pangani wataunga mkono kwa dhati maslahi ya nchi na wajibu wao katika Sekta ya Maji
iv. Kutopendelea
Wafanyakazi wa Bonde la Pangani watazingatia haki na usawa katika kutoa huduma na kushughulikia wateja