Huduma ya utafiti wa kijiofizikia na kihaidrojiolojia inafanywa kwa lengo la kutafuta maji chini ya ardhi, Utafiti huu unajumuisha njia mbili ambazo ni njia ya umeme na njia inayohusisha usumaku. Njia inayohusisha usumaku inasaidia kutafuta mikondo ya maji iliyo hai na iliyokufa ambayo inapatikana chini ya ardhi, Njia ya pili ni njia ya umeme hii inasaidia kujua umbali wa mikondo ya maji iliyoko chini ya ardhi.
Bodi ya maji ya bonde la Pangani inatoa huduma hii kwa makampuni, taasisi za serikali, taasisi zisizo za kiserikali na kwa mtu mmoja mmoja. Utaratibu wa kupata huduma hii ni rahisi ambapo mteja ataiandikia barua ya maombi kwenda kwa mkurugenzi wa bodi ya maji, na itajibiwa kwa haraka iwezekanavyo na mteja atapewa makadirio ya gharama za huduma hii.