Uhamasishaji wa Jami...
Uhamasishaji wa Jamii kwa ajili ya Uhifadhi wa Mto Pangani
18 Jun, 2022
Uhamasishaji wa Jamii kwa ajili ya Uhifadhi wa Mto Pangani

Bodi ya Maji Bonde la Pangani imeendelea na uhamasishaji katika vijiji vilivyopo kando ya Mto Pangani ambapo tarehe 14 June 2022 wataalamu toka Bodi ya Maji Bonde la Pangani wamefanya mikutano na wananchi katika Mji Mdogo wa Korogwe kwenye mitaa ya Old Korogwe, Kwazomolo, Lwengera Railway na Lwengera Darajani na kutoa elimu kuhusu ushiriki wa jamii katika uhifadhi na utunzaji wa rasilimali za maji ambapo tayari wananchi zaidi ya 800 wamepatiwa elimu ya masuala ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji. Hata hivyo kwa kiwango kikubwa changamoto nyingi za uchafuzi hutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo shughuli za majumbani za uoshaji na ufuaji. Aidha katika maeneo takribani yote Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza miradi ya maji katika hatua mbalimbali na hivyo kuleta matumaini makubwa ya kunusuru uchafuzi wa Mto Pangani usababishwao na shughuli za kibinadamu. Pichani ni wataalamu toka Bodi ya Maji Bonde la Pangani kwa kushirikiana na RUWASA Korogwe, Mamlaka ya Maji KUWASA, Halmashauri za Wilaya ya Korogwe na Muheza. Bodi ya Maji Bonde la Pangani inasisitiza wananchi kujitokeza kushiriki Sensa ya Watu na Makazi kufanikisha mipango ya utunzaji na matumizi ya rasilimali za maji. UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI NI JUKUMU LETU SOTE