Maadhimisho ya Wiki ya Pangani
Bodi ya Maji Bonde la Pangani inasimamia eneo bonde lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 54,600 ambayo ni asilimia 93% ya Bonde zima na asilimia 7% iko Nchini Kenya inayolifanya Bonde letu kuwa ni la kimataifa. Pia linalohusisha Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara katika Halmashauri za Wilaya takribani 24. Bonde la Pangani lilianzishwa mnamo Julai 1, Mwaka 1991 na mwaka huu tarehe 1 Julai 2022 linatimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake. Ili kuazimisha miaka 31 tangu kuanzishwa kwa Bonde la Pangani, Bodi imeandaa program mbalimbali ambazo zimeanza leo tarehe 25 Juni, 2022 na programu hizi zitakuwa kwa wiki nzima ambapo hitimisho lake litakuwa ni tarehe 1 Julai 2022.
Program mbalimbali zilizoandaliwa ni Pamoja na maonyesho ya shughuli mbalimbali za Bonde la Pangani ambapo kwa Mkoa wa Kilimanjaro yatafanyika katika Soko la Manyema lililoko katika Manispaa ya Moshi, Kwa Mkoa wa Arusha yatafanyika katika Ofisi za Maji Bonde la Pangani zilizoko Barabara ya Wachaga na kwa Mkoa wa Tanga yatafanyika katika Ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Pangani zilizoko Barabara ya Gofu. Pia tumeandaa program za kusafisha vyanzo vya Maji ambapo wananchi wataweza kushiriki katika shughuli za usafishaji wa Vyanzo vya Maji na kupata elimu ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji.
Bodi ya Maji Bonde la Pangani inawakaribisha wote kushiriki katika maadhimisho haya
“Utunzaji wa Vyanzo vya Maji ni Jukumu Letu Sote”