Kamati ya ulinzi na Usalama Wilayani handeni yapewa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji
Kutokana na kukua kwa matumizi ya maji katika maeneo mbalimbali kwenye Bonde la Pangani, Bodi imeendelea kupokea na kutatua migogoro mbalimbali ya matumizi ya maji hususani ihusuyo matumizi ya maji majumbani pamoja na kilimo ambapo migogoro mingi hutokana na upungufu wa maji hususani wakati wa kiangazi. Pichani ni kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya maji kati ya Kijiji cha Maksoro (ukanda wa juu) na vijiji vya Marurani, Manyire na Mlangarini (ukanda wa chini) ambavyo hutumia maji ya Chemchemi ya Machumba iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha. Zoezi hilo lilianza kwa kutembelea chanzo husika na kufanya kikao cha pamoja ambapo makubaliano ya utatuzi yalifanyika kwa mafanikio kwa kukubaliana kurudisha maji katika banio (intake), kuboresha miundombinu na kudhibiti uharibifu wa chanzo utokanao na shughuli za kibinadamu. Kikao hicho kilihudhuriwa na RUWASA Wilaya ya Meru, Jumuiya ya Watumia Maji Mto Nduruma, Watendaji wa Kata za Akheri, Ambureni na Nduruma pamoma na vijiji na vitongoji husika. Kikao hicho kilifanyika tarehe 07.09.2022 kwenye eneo la wazi katika Kijiji Shangarai kitongoji cha Machumba ambapo ndipo ilipo Chemchemi ya Machumba.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel S. Mchembe akisisitiza jambo wakati wa elimu ya uhifadhi wa vyanzo vya maji
Picha ya Pamoja ya Kamati ya Ulinzi na Usalama na Watumishi wa Bodi ya maji Bonde la Pangani baada ya elimu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji