Bonde la Pangani Latembelea Kituo cha Watoto Yatima
Katika kuadhimishia Wiki ya Bonde la Pangani, Bodi imetembelea kituo cha watoto yatima kilichopo katika Manispaa ya Moshi kama ishara ya kuwajali watoto waishio katika mazingira magumu, kutoa msaada pamoja na kuongeza mwonekano wa taasisi katika kukuza uelewa na umuhimu wa kutunza na kuhifadhi rasilimali za maji. Katika maadhimisho hayo Bodi imetembelea kituo cha watoto yatima cha Halima Selengia kilichopo katika Manispaa ya Moshi tarehe 29 Juni 2022 na kuwapatia mahitaji mbalimbali kama sehemu ya mchango wake na kuonyesha namna ambavyo Bodi ipo karibu wanajamii katika kutekeleza na kufanikisha majukumu yake. Bodi ya Maji Bonde la Pangani kama zilivyo Bodi nyingine za Mabonde inaendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika utunzaji wa vyanzo vya maji ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa taifa letu.
Pichani ni baadhi ya watumishi wa Bodi (waliosimama kwa nyuma) wakiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mto Rau (mwenye reflective jacket) wakiwa na watoto wa kituo hicho pamoja na matukio mengine ya pamoja wakati wa kukabidhi msaada kwa watoto wa kituo hicho.